uwoya atoa somoo

MSANII mahiri wa filamu Tanzania, Irene Uwoya, amesema kuwa tasnia ya filamu itakuja kupata heshima kubwa endapo wasanii wenyewe watajiheshima kupitia maisha yao pamoja na kazi wanazotoa.

Msanii huyo amepata sifa baada ya kushiriki katika filamu kadhaa hasa zile ambazo zinampa uwezo mkubwa wa kuonesha hisia za kimapenzi.

Akiongea na drop ent.., Uwoya alisema kuwa wasanii wanalilia heshima lakini wenyewe hawana heshima kitu ambacho hakina maana yoyote kwani hawajui kitu kinachowanyima heshima hiyo.

Alisema kuwa wanapenda kuishi kama nyota wakubwa wa Ulaya, ambao wamekuwa wakipewa heshima kubwa, ingawa hawajui ni kitu gani ambacho kinawapa nafasi ya kuheshimika mbela ya jamii inayowazunguka.

“Wasanii wa nje wanaheshimika kwanza kazi zao ni nzuri, sisi huku tunatoa filamu moja tena mbaya halafu tunalilia kupewa heshima nani kasema, tufanye kazi baadae kila kitu kitakuja,” alisema.

Aliongeza kuwa kuna nyota wengi wa Ulaya ambao ni matajili hivyo hata heshima wanayoipata ni kutokana na utajili wao pamoja na kazi nzuri wanazotoa amabzo zinatazamwa duniani kote.

“Msanii huwezi kupata heshima wakati wewe mwenyewe hujiheshima na kitu hiki ndicho kinachosumbua wasanii wengi, pia wanataka kuishi maisha kama wasanii wa nje wakati kazi zao mbaya kitu ambacho hata ikiwa sokoni haiwezi kufanya vizuri,” alisema.

Comments