wema sepetu aamua kufanya kazi

BAADA ya mikasa kibao msanii Wema Sepetu, amesema kuwa kwa sasa anaamua kutulia na kufanya kazi kwani katika harakati zote alizopitia hakuna hata moja ilimfanya aonekane mwame zaidi kumjichafulia jina lake.

Msanii huyo alidai kuwa watu wengi wamekuwa wakimuona muhuni na mara nyingine anapopita sehemu hujikuta akitolewa macho na watu.

Aliongeza kuwa kwa sasa haitaji kuonekana mara kwa mara sehemu za starehe kwani huko ndiko kunakotokea mambo ya ajabu ambapo huwa anashindwa kujizuia na kujikuta amefanya baada ya kulewa.

“Mimi nikilewa huwa mbaya sana na naweza kufanya kitu na baada ya muda nikaja kujuta ni kwanini nimefanya ila kwa sasa naweza kusema najiweka bize na mambo yangu,” alidai Wema.

Comments