dogo janja arudi darr kwa mbwe mbwe arudi na ndege ma mia yajitokeza kumpokea

Dogo Janja ambae alisema amefurahishwa na hayo mapokezi na kusisitiza kwamba japo aliapa hatorudi kuja kusoma Dar wazazi wake wamemsihi kwamba zile zilikua hasira tu hivyo arudi Dar na aedelee na masomo kitu ambacho amekikubali kwa roho safi. 

Janja amesema bado hajasaini mkataba mpya na WATANASHATI lakini kuna watu wake wawili anaowasubiri kwa ajili ya kuja kuupitia pamoja huo mkataba, baada ya hapo ndio atasaini kama amekubaliana nao na atatangaza. 

Amesema amebadili mawazo na sasa atasoma Dar es salaam katika shule nzuri ambayo aliahidiwa na Ostaz Juma meneja wa Watanashati, atakua anapelekwa shule na kurudishwa nyumbani kwa gari, anachohitaji pia ni kusoma kwenye shule binafsi nzuri na pia swala lake la muziki kuzingatiwa. 

kwenye sentensi nyingine amesema “sasa hivi nitakua naigiza na filamu pia na kina Kitale manake tuko nao kwenye kundi moja la watanashati”

Kwa kumalizia Janja amesema kauli mbiu ya wakati huu imebadilika “kauli mbiu ya wakati nilivyokujaga nilisema nawakalisha matembo sasa hivi nawalaza chali matembo”


Dogo Janja atasikika kwenye AMPLIFAYA ya CLOUDS FM kuanzia saa moja leo usiku utapata nafasi ya kusikia alichosema na jinsi alivyopokelewa kwa shangwe.
sorce =djchoka na millardayo.com

Comments