mastaa wanao itwa baba hapa bongo







Haijalishi kama wao ni marapper wagumu ama wasanii wenye mlolongo wa show ama kazi zinazowafanya wasiwe karibu na familia, hakuna anayeweza kupinga kuwa watu maarufu huvutia zaidi wawapo baba.
Ni heshima kubwa wanapoonekana wakicheza na watoto wao ama kupiga picha za pamoja wakiwa na nyuso za furaha kuashiria kuwa wanaenjoy majukumu ya ubaba.
Wakati jana ilikuwa ni siku ya baba (Father’s Day) bongo5 inapenda kuwatambua baadhi ya watu maarufu nchini waliopiga picha na watoto wao.
Kama una wasiwasi kuwa baba, ama mtoto uliyeambiwa ni wako humtaki, waulize hawa Baraka na Furaha inayotokana na kuwa baba unayewajibika.
Hawa ni miongoni mwa nyota wa Tanzania vijana waliotoka kwenye status ya kuwa masela na kuwa Baba. Wapo wengine wengi lakini kwa sasa ni hawa tuliofanikiwa kupata picha zao.
1. Raqey Mohammed
Ni miongoni wa wapiga picha mahiri kabisa nchini Tanzania. Anafanya kazi kwenye kampuni ya i-view media Ltd kama Creative Consultant, Film Making,Storyboard, Script writing na Direction. Kazi zake zimeonekana kwenye matangazo ya makampuni makubwa nchini. Mwanae anaitwa Raqsah aliyezaa na mke wake Sarah Soso Raqey.
2. Hamis Mwinjuma aka MwanaFA
Toka enzi za Ingekuwa vipi na Mabinti Damu Damu, MwanaFA Hajakoma kuandika nyimbo zenye mashairi makali yenye maana kubwa. Pamoja na kudai kuwa muda wa kuoa bado sana kwake, alipenda kwanza kuwa baba na kumleta duniani binti mrembo aitwaye Maleeka.
3. JCB
Mtengwa JCB aliamua kuchanganya rangi na mke wa kizungu na kufyatua mtoto aliyechukua weupe wa mama yake. Sasa pamoja na kuendelea kufanya hip hop ngumu kama kawaida yake, kila anaposikika watu huvuta picha ya mwanae na kutambua kuwa licha ya mistari mizito, JCB ni baba anayewajibika.
4. Banana Zorro
Akiwa ameshakuwa mzoefu kwenye maisha ya ndoa, Banana Zorro haoni tabu tena ya kuwa baba zaidi ya furaha tele na mapenzi mazito kwa familia yake.
5.Soggy Doggy
Ukimwona mjini unaweza usifikirie kuwa huko nyuma kuna binti mrembo ambaye ni mwanae na anayemtegemea maishani. Soggy ana kila sababu za kujivunia kumkuza Alexsandra, mwanae wa kike.
6. Dully Sykes
Mzee wa Misifa aliona kuwa umri unaenda na haina maana tena kuendeleza misifa wakati hana hata mtoto wa kusingiziwa na ndipo alipoamua kujitumumua na kulizingatia agizo la mwenyezi Mungu la kwamba tuje duniani tuzaliane.
7. Nikki Mbishi
Rais wa wabishi na miongoni wa mamc wakali kabisa kuwahi kutokea nchini Nikki Mbishi, aliamua kumuita mwanae wa kiume jina la role Model wake Malcom X.
8. Mike T
Pamoja na scandal za hivi karibuni zilizomwandama, Mike T ameendelea kuwa jasiri na baba mwenye kuzingatia wajibu wake katika familia inayomtegemea. source
by bongo5.com

Comments