usichokijua kuhusu ommy dimpoz

Mawazo ya kuwa maisha mazuri yapo Ulaya hayakuwa mageni kwa Faraji Omar Mgimbo aka Ommy Dimpoz.
Mipango yake akiwa shuleni ilikuwa ni kutafuta njia yoyote iwezakanayo, iwe halali ama haramu ili afike Ulaya na mengine yangejulikana huko huko.
Dimpoz kwa pozi kama anavyopenda umuuite, aliamini kuwa akifika Ulaya, nchi yoyote, atapata kazi, hata kama ni kazi ya ndani ama kubeba box, ilimradi tu yupo Ulaya.
Lakini baada ya muda kwenda, kijana huyu mwenye asili ya mkoa wa Kigoma wazo la kuzamia majuu likaanza kuyeyuka na kulipisha wazo jingine la kutafuta maisha katika muziki.
Kama aliyeongozwa na Malaika kujaribu bahati yake katika muziki kwa kuanzia na uimbaji wa bendi, leo hii Ommy Dimpoz ni msanii asiyekoswa kutajwa na mashabiki wa muziki nchini.
Akianza na Nai Nai aliyomshirikisha Ali Kiba, watu walidhani labda wimbo huo umehit kwasababu kamshirikisha staa wa Cinderella.
Akiongena na kipindi cha Power Jams cha East Africa Radio jana, amesema hata yeye mwenyewe wimbo huo aliuchukulia poa na mpaka leo umemfikisha hapo alipo, haamini.
Akiwa miongoni mwa wasanii waliong’ara kwenye tuzo za Kili 2012, Ommy Dimpoz amewaziba mdomo watu waliodhani kabahatisha kwa kutoa club banger inayotikisa kwa sasa nchini iitwayo Baadaye.
Wimbo huo wenye ladha ya kinaijeria na uliotenengenezwa na Man Walter wa Combination Sounds, umegeuka kuwa anthem kwenye vituo vya radio na mtaani.
Habari njema kwa mashabiki waliotekwa na Baadaye ni kuwa yupo kwenye hatua za mwisho kabisa kuanza kushoot video ya wimbo huo ambayo anasema itakuwa kali pasipo mfano.

Comments