shamsa ford kitumbo kinamsumbua

uJAUZITO wa msanii Shamsa Ford, umezidi kuleta matatizo makubwa ndani ya familia yake, kwani kwa sasa hataki kujihusisha na kitu chochote kwa madai kuwa anaumwa.

Mmoja wa wanafamilia ya msanii huyo aliyezungumza na drop aliyejitambulisha kwa jina moja la Peter, alisema kuwa kitu kikubwa ambacho wamekuwa wakisumbuana naye ni uvivu kwani hata kufua nguo zake inakuwa mtata.

Alidai kuwa pamoja utata huo bado hataki kufanya mazoezi kitu ambacho hata wazazi wake wamekuwa wakisikitika juu ya hilo.

“Unajua hii ndo mimba yake ya kwanza hivyo bado hajaelewa nini anachotakiwa kikufanya ili kuweza kufanya mazoezi, hivyo kuna mtu wa mshauri ambaye anatarajia kuletwa nyumbani kwa ajili ya kuzungumza naye.

Hata hivyo mwandishi wa drop alimtafuta msanii huyo na kuzungumza naye juu ya kero hiyo ndani ya familia yake, ambapo mwenyewe alisema kuwa huwa anajisikia uvivu kufanya kazi yoyote ile.

Alisema kuwa mara zote amekuwa akilala na muda wa jioni huwa anafanya mazoezi kwa ajili ya kujenga mwili wake ingawa hakuwa hapendi kufanya kitu hicho

Comments