dogo janja arudi darr kwa mbwe mbwe arudi na ndege ma mia yajitokeza kumpokea
Dogo
 Janja  ambae alisema amefurahishwa na hayo mapokezi na kusisitiza 
kwamba japo  aliapa hatorudi kuja kusoma Dar wazazi wake wamemsihi 
kwamba zile  zilikua hasira tu hivyo arudi Dar na aedelee na masomo kitu
 ambacho  amekikubali kwa roho safi. 
Janja
 amesema bado hajasaini  mkataba mpya na WATANASHATI lakini kuna watu 
wake wawili anaowasubiri  kwa ajili ya kuja kuupitia pamoja huo mkataba,
 baada ya hapo ndio  atasaini kama amekubaliana nao na atatangaza. 
Amesema
 amebadili mawazo na  sasa atasoma Dar es salaam katika shule nzuri 
ambayo aliahidiwa na Ostaz  Juma meneja wa Watanashati, atakua 
anapelekwa shule na kurudishwa  nyumbani kwa gari, anachohitaji pia ni 
kusoma kwenye shule binafsi nzuri  na pia swala lake la muziki 
kuzingatiwa. 
kwenye
  sentensi nyingine amesema “sasa hivi nitakua naigiza na filamu pia na 
 kina Kitale manake tuko nao kwenye kundi moja la watanashati”
 
Kwa
 kumalizia Janja amesema  kauli mbiu ya wakati huu imebadilika “kauli 
mbiu ya wakati nilivyokujaga  nilisema nawakalisha matembo sasa hivi 
nawalaza chali matembo”
 
Dogo
 Janja atasikika kwenye  AMPLIFAYA ya CLOUDS FM kuanzia saa moja leo 
usiku utapata nafasi ya  kusikia alichosema na jinsi alivyopokelewa kwa 
shangwe.
sorce =djchoka na millardayo.com 



Comments
Post a Comment