kisa cha dogo janjaa kutimuliwa tip top connection

DOGO JANJA ATUPIWA VIRAGO TIP TOP CONNECTION


Nyota wa muziki wa kizazi kipya kutoka ‘kruu’ ya Tip Top Connection yenye maskani yake pande za Manzese jijini Dar es Salaam Abdul Abubakar Chende ‘Dogo Janja’ ametupiwa 
virago ndani ya kundi hilo.

Akizumngumza na Teentz .com mapema leo kiongozi wa kundi hilo Hamad Ally ‘Madii’ amesema kuwa Dogo Janja ameshindwa kuendana na makubaliano halisi yaliyokuwepo baina yake na uongozi wa kundi hilo ikiwemo kuhudhuria shuleni kama alivyokuwa akitakiwa kufanya kila siku badala yake amekuwa akiendekeza starehe na wakati mwingine kufanya mambo ambayo kwa namna moja ama nyingine yalikuwa yanalichafua kundi hilo.

“Tumemkabidhi kwa kaka yake mapema leo tukiwa maeneo ya Ubungo tayari kwa safari ya kurudi kwao na wakati huo tulifanya mawasiliano na baba yake kumuarifu kuwa Tip Top hatuko na mwanae kwa sasa” alisema Madii

Katika hatua nyingine Madii amesema kuwa Dogo Janja alilewa sifa na kujisahau kufanya yale anayotakiwa kufanya ndani nanje ya kundi kufuatia mafanikio ya muziki aliyoyapata akiwa na Tip Top Connection kwani hivi karibuni alitega shule na kwenda kujificha nyumbani kwa TundaMan hukua akimuaga Madii kuwa anakwenda shule.

Kuona hivyo TundaMan aliamaua kumuarifu Madii na mara moja kiongozi huyo wa kundi aliamua kwenda kumsaka, lakini baada ya dogo Janja kugundua kuwa Madii anakuja aliamua kukimbia na kwenda kujificha uchochoroni lakini akiwa huko mafichoni bahati mabaya alikanyaga kuku na siri yake kujulikana kuwa amejificha hapao ndipo alipokamatwa na kuamriwa kufungasha kilicho chake tayari kurejea ‘kileji’.

"vimekuwa ni vitendo vya kila mara kukacha kuhudhuria shule, tumechoka na hatukuwa na njia nyingine ya kufanya alisema Madii'

Comments